Ijumaa , 13th Sep , 2019

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, amesema yupo tayari kukatwa mkono endapo mshambuliaji David Molinga  hatafikisha magoli 15, kwenye ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu.

Mwinyi Zahera

Zahera amesema hayo alipokuwa akiongelea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia, utakaopigwa Jumamosi Septemba 14, kwenye uwanja wa taifa.

Kauli hiyo ya Zahera imekuja baada ya mashabiki kuonekana kutoridhishwa na kiwango cha mshambuliaji huyo, aliyesajiliwa msimu huu akitokea DR Congo.

Zaidi tazama Video hapo chini.