Akizungumza na EATV/ EA Radio Digital Meya wa Temeke, Abdallah Chaulembo, amesema 2 ya 3 ya Madiwani wa jiji hilo, wamekubaliana na hoja hiyo, na wameiwasilisha kwa Mkurugenzi wa jiji tangu, Septemba 5, 2019.
Chaulembo amesema kuwa "ni kweli tumesaini hoja ya kumtuhumu na kutokuwa na imani na yeye, ukisoma kanuni inajieleza sababu kwamba kama hamtakuwa na imani na yeye ni sawa kuandika hiyo hoja, na kanuni inasema 2 ya 3 Madiwani na sisi tumefika"
"Barua tumeandika toka tarehe 5, mwezi 9 na tulimpa Mkurugenzi na kama ilimfikia Mkurugenzi siku hiyo hiyo, maanake siku 5 zimeisha" ameongeza Chaulembo
Juhudi za kumtafuta Meya Isaya Mwita, ziligonga mwamba kutokana na simu yake kuita bila kupokelewa.
Mara baada ya kuwasilisha kwa utetezi wake, Mkurugenzi wa jiji anatarajia kuufikisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ambaye yeye ataunda kamati ya kuchunguza tuhuma zake, ambapo kama ikithibitika anahatihati ya kupoteza nafasi yake.

