
Nchimbi ni mmoja ya washambuliaji wachache kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambao wanatambulika kwa uwezo wa kupambana na mabeki kwa mipira ya juu na chini, akitarajiwa kuongeza kitu katika eneo la ushambuliaji la Azam FC.
Zoezi la uingiaji mkataba baina ya pande hizo mbili limesimamiwa na Meneja wa timu hiyo, Phillip Alando, ambaye ameweka wazi kuwa ujio wa mshambuliaji huyo ni kuboresha eneo la ushambuliaji.
Huo ni usajili wa tatu kwa Azam FC kuelekea msimu ujao, awali ikitangulia kuwasajili nyota wawili kutoka Zimbabwe mshambuliaji Donald Ngoma na kiungo Tafadzwa Kutinyu, wote wakipendekezwa na Kocha Mkuu mpya, Hans Pluijm.