
Daktari Mwanandi amesema kuwa wachezaji Yakubu Mohamed, Daniel Amoah, Ladislaus Stanslaus, Waziri Junior na Donald Ngoma wanaendelea na matibabu na wengine wameshapona na kuanza mazoezi mepesi.
Amesema Yakubu Mohamed ambaye alivunjika mguu kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Combine mwezi Februari, alitibiwa nchini Afrika Kusini na ameshapona akiwa ameanza mazoezi tangu Juni 1.
Kwa upande wake mlinzi Daniel Amoah ambaye aliumia goti kwenye mechi dhidi ya Simba, anaendelea na matibabu na sasa yupo kwenye hatua ya kuanza mazoezi taratibu lakini itamchukua miezi 9 kurejea uwanjani.
Wachezaji Waziri Junior na Ladislaus Stanslaus ambaye alikuwa Costal Union kwa mkopo wanaendelea na matibabu ambapo hivi karibuni watapelekwa Afrika Kusini kwaajili ya matibabu zaidi.
Mshamabuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma aliyesajiliwa kutoka Yanga, amefanyiwa vipimo na matibabu nchini Afrika Kusini na ameambiwa ataanza kucheza mwezi Agosti. Aidha Azam FC wameweka wazi kuwa walikuwa wanasubiri ripoti ya vipimo ili waweze kuona kama watamsajili.