Jumanne , 15th Jul , 2014

Msanii nyota wa Nigeria 2Face Idibia anatarajia kudondosha solo albam yake ambayo ni ya sita iliyobatizwa jina 'THE ASCENSION' ambayo itatolewa rasmi mwezi huu.

msanii 2Face Idibia wa Nigeria

Tuface ameelezea kuwa albam yake hiyo itabeba nyimbo 17 ambazo amewahakikishia mashabiki kuwa zitakuwa moto wa kuotea mbali.

Mkali huyo tayari amefyatua single ya wimbo mpya kutoka ndani ya albamu yake uliobatizwa jina ‘Let Somebody Love You’ akimshirikisha msanii Bridget Kelly.