Jumanne , 3rd Jun , 2014

Mshindi wa tuzo ya Oscar wa Kenya Lupita Nyong'o pamoja na nyota wa filamu ya Game Of Thrones, Gwendoline Christie ni miongoni mwa waigizaji wapya waliopata dili la kujiunga hivi karibuni katika upigaji picha ya filamu mpya ya Star Wars VII.

Lupita akitabasamu kuchaguliwa kuigiza

Lupita aliyetwaa tuzo kutokana na kushiriki vyema kwenye filamu ya '12 Years A Slave' ataungana na nyota wengine katika filamu hiyo mpya itakayoongozwa na J.J. Abrams.

Shavu hili linatarajia kuendelea kun'garisha zaidi nyota ya Lupita katika anga la kimataifa, akiwa sasa anang'ara katika filamu mpya ya Non Stop ambayo uhusika mkuu ndani yake unavaliwa na Liam Neeson.