
Anthony Davis
Awali Davis aliweka wazi kabla ya mchezo huo maalum wa NBA, maarufu kama All-Star Game usiku wa kuamkia leo, kuwa alipania kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo, maarufu kama MVP, ahadi ambayo ilitimia
Nyota huyo wa Pelicans amefanikiwa kuvunja rekodi ya ufungaji ya mchezo huo ya pointi 42 iliyowekwa na Wilt Chamberlain mwaka 1962.
Mchezo wa NBA All-Stars huchezwa kila mwaka kati ya sehemu ya Magharibi na sehemu ya Mashariki mwa nchini Marekani na mwaka huu, mchezo huo ulichezwa katika Uwanja wa Smoothie King ambao ni uwanja wa nyumbani wa timu ya Pelicans.