Shamba la bangi pamoja na mafurushi ya bangi yaliyokuwa nyumbani kwa mtuhumiwa
Kamanda wa Polisi Mkioa wa Mbeya DCP Dhahiri Kidavashari amesema tukio hilo limetokea tarehe 16 Februari mwaka huu na kumtaja mtu huyo kuwa ni Upe Nduta mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa Jojo Wilaya ya Kipolisi ya Mbalizi, ambaye alikuwa amelima shamba lenye ukubwa wa ekari moja.
Aidha katika Oparesheni hiyo zaidi ya miche 2,000 iliyokomaa ilikutwa shambani kilogram 2 na gram 145 za bangi pia zikikutwa nyumbani kwake.
Kamanda Kidavashari amesema mtu huyo muuzaji/msafirishaji na mtumiaji wa dawa za kulevya .
Katika hatua nyingine, kwa nyakati tofauti, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekamata watuhumiwa wanne wakiwa na dawa za kulevya aina ya bangi misokoto mitatu yenye uzito wa kilogram 15 na gram 685 kati ya tarehe 11 Febriari hadi 16 Februari, 2017.