Alhamisi , 1st Dec , 2016

Msanii Vanessa Mdee ambaye yupo kwenye kinyang'anyiro cha mwanamuziki bora wa kike kwenye Tuzo za EATV, amesema anajiona mwenye ubora kwa kufanikiwa kupenya kwenye kipengele hicho.

Vanessa Mdee

 

Akizungumza na EATV, Vanessa Mdee amesema kipengele hicho ni kigumu sana kwake kutokana na wasanii wengine wa kike waliopo kuwa na uwezo mkubwa, hivyo imekuwa changamoto kubwa kwake.

"Nomination yangu niliipata nikiwa South Africa nilikuwa ziarani, ilikuwa habari nzuri kupata nikiwa huko makazini, category ni ngumu sana obviously wana dada wote wanastahili kwa sababu wanafanya kazi nzuri sana, nawaheshimu nawapenda wote na mimi ni shabiki wao wote, kuwepo tu kwenye hiyo category inaonesha nina ubora na ninastahili, kwa hiyo nikisema mimi ni bora kupita wengine nitakuwa nakosea kwa sababu kila mtu anastahili", alisema Vanessa Mdee

Pia Vanessa Mdee amesema anautamani sana usiku wa EATV AWARDS, ili kuweza kukutana na wasanii wenzake ambao mara nyingi amekuwa akikosa muda wa kuonana nao pamoja na wadau wa muziki, lakini kikubwa tayari amesha andaa hadi vazi la kuvaa siku hiyo.

Wanaowania tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike pamoja na Vanessa Mdee

"I love awards, nikienda kwenye tuzo napenda kwanza ni nafasi ya kuonana na wadau wa muziki, wasanii wenzangu ambao sometimes sipati nafasi ya ku'hang' nao kuonana nao, kuwa nao karibu natamani kuona red carpet flan amazing, watu wamependeza,  watu wanakuja ku'suport' muziki wa Tanzania, ni hatua nyingine tena kwetu sisi ambao tunapigana kila siku kuboresha mziki wetu na sanaa yetu, i'm excited nimeshafikiria nguo na kupangilia vazi la kuvaa and you know i cant wait", alisema Vanessa Mdee

Kupiga kura ingia hapa www.eatv.tv/awards

Tags: