
Gareth Southgate
Kocha huyo, wa zamani wa kikosi cha Uingereza chini ya umri wa miaka 21, amepewa kibarua cha muda baada ya kufukuzwa kazi Sam Allardyce, aliyeiongoza timu hiyo kwa siku 67 pekee.
Southgate, amesema bado hajui kama atapewa kazi, lakini anaamini kabla ya mwezi huu kuisha, kila kitu kitajulikana, lakini vyanzo mbali mbali vya habari nchini Uingereza, vimedokeza kuwa FA ina mpango wa kumpa mkataba wa miaka 4, wenye thamani ya pauni milioni mbili kwa mwaka, na mazungumzo hayo, yanatarajiwa kuanza mara baada ya mchezo wa kirafiki, dhidi ya Hispania usiku wa leo katika Uwanja wa Wembley.