Jumapili , 6th Nov , 2016

Mgombea urais wa Marekani Donald Trump amejikuta akiondolewa haraka jukwaani huko Nevada na maafisa usalama kwa kuhofia usalama wake.

Donald Trump akiondolewa jukwaani na afisa usalama baada ya kudaiwa kuwepo tishio la usalama wake.

Mgombea wa urais wa Marekani wa chama cha Republican, Bw. Donald Trump, amejikuta akiondolewa haraka jukwaani na maafisa usalama katika mkutano wake wa hadhara huko Reno, Nevada kwa kuhofia usalama wake.

Hofu hiyo imetokana na mwanaume mmoja aliyekuwa amebeba bango lililoandikwa Republican hawamuungi mkono Trump, kudaiwa kuwa na silaha hata hivyo alipokamatwa na maafisa usalama ilibainika kuwa hana silaha.

Hata hivyo Bw. Trump alirejea jukwaani baada ya kuhakikishiwa usalama wake, na kueleza kuwa amejipanga kwenda kwenye majimbo ambayo ni ngome kuu ya chama cha Democratic cha mgombea urais Bi. Hillary Clinton.