Jumamosi , 5th Nov , 2016

Wachezaji wa timu ya taifa ya Zimbabwe watakaochuana na Tanzania (Taifa Stars) katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaopigwa Novemba 13 mwaka huu nchini humo, yamewekwa hadharani.

Shirikisho la Soka nchini Zimbabwe

Wachezaji hao ni makipa: Tatenda Mukuruva (Dynamos) na Donovan Bernard (How Mine).

Mabeki: Godknows Murwira (Dynamos), Hardlife Zvirekwi (CAPS United), Ronald Pfumbidzai (CAPS United), Honest Moyo (Highlanders), Lawrence Mhlanga (Chicken Inn) na Teenage Hadebe (Chicken Inn).

Viungo: Tendai Ndlovu (Highlanders), Farai Madhanhanga (Harare City), Jameson Mukombwe (Chapungu), Tafadzwa Kutinyu (Chicken Inn), Ronald Chitiyo (Harare City), Talent Chawapihwa (ZPC Kariba) na Malvern Gaki (Triangle).

Washambuliaji: Pritchard Mpelele (Hwange), Gift Mbweti (Hwange), Leonard Tsipa (CAPS United), Rodreck Mutuma (Dynamos) na William Manondo (Harare City)

Akizungumza kwa niaba ya Kocha Mkwasa, Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema iwapo Taifa Stars itafanikiwa kushinda mchezo huo itaiweka Tanzania katika nafasi nzuri katika viwango vya ubora vya FIFA.