Rammy Galis akiwa Kikaangoni
Galis ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu namna alivyopokea hatua ya kuanzishwa kwa tuzo hizo.
“Ukweli nilifarijika sana kusikia tuzo hizi ambazo zinaandaliwa na kituo cha habari na zaidi ya yote kituo ambacho kinajihusisha na wasanii moja kwa moja kwa kusaidia kazi zisonge mbele, hivyo tuzo hizi zitasaidia sana kujenga hamasa ya ushindani nchini” Amesema Galis.
Aidha Galis amesisitiza kwamba yeye amesharejesha fomu za kujipendekeza kwenye tuzo hizo anachosubiri ni hatua nyingine zitakazo tangazwa na kituo kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa upatikanaji wa tuzo hizo.
Aidha msanii huyo amewataka wasanii ambao hawakujitokeza kushiriki kwenye tuzo hizo waendelee kufanya kazi nzuri na zinapotangazwa tuzo kama hizo waweze kujitokeza kwani msanii akipata tuzo humsaidia sana kupaa kitaifa na kimataifa kulingana na uzito wa chombo kinachotoa tuzo na uzito wa tuzo zenyewe.