
Akizungumza kwenye Stori 3 za Planet Bongo ya East Africa Radio, M Rap Lion amesema tangu ameanza kufanya muziki amekuwa na ndoto kubwa ya kufanya muziki utakaojulikana kimataifa, bila kujali lugha kwani muziki wenyewe ni lugha ya ulimwengu wote, bali ni ubunifu ndiyo unaohitajika.
"Naweza nikasema mind set yangu mi ni kubwa kuliko watu wengine, mi nawaza zaidi kukamata soko hata la West Afrika, nikamate soko la Asia, lakini mtu anaweza akajiuliza hiyo inawezekana vipi, 'music is a universal language', yani muziki haujalishi hata mtu uimbe wimbo gani ukiwa na vitu flan ambavyo ni catch mtu yeyote lazima vimkamate na muziki wako lazima utanunuliwa", alisema M Rap Lion.
M Rap aliendelea kwa kusema ...."Tangia naanza muziki nimekuwa nikijengea kwamba mimi nataka nifike to the world, nataka nijulikane kila sehemu siyo Tanzania tu, nataka nijulikane Kenya, Uganda, Rwanda, nimekuwa nikifanya hivyo tangu siku ya kwanza kwa hiyo so far ni suala ambalo lipo katika akili yangu", alisema M Rap.
Suala la muziki wetu kwenda kimataifa wasanii wengi wamekuwa wakitoa sababu ya kutojua lugha ambazo nchi mbali mbali wanaongea, kitu ambacho M Rap Lion ametazama kwa mtazamo tofauti.