Alhamisi , 18th Aug , 2016

Wasanii mbalimbali nchini wameonesha kuzifurahia tuzo zilizoanzishwa na East Africa Television na kusema zimekuwa mkombozi mkubwa kwao.

Fid Q

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, msanii Fid Q alisikika akisema kwa niaba ya wasanii wenzake wamefurahia kitendo hicho, na wameishukuru East Africa Television kwani waliteseka kwa muda mrefu.

"Tunaishukuru sana East Africa TV kwa kuanzisha hizi tuzo, ki ukweli wasanii tuliteseka sana kwa kuwa na tuzo moja kwa muda mrefu, lakini sasa tumepata na ni kitu kikubwa kwenye industry, tunaushukuru uongozi mzima kwa kuja na hili", alisema Fid Q.

Licha ya hayo, wasanii wengine wameonesha kufurahishwa kwao kwa tuzo hizo na kuandika kwenye mitandao ya kijamii, wakielezea hisia zao. Na hiki ndicho baadhi ya wasanii waliandika:

Walichopost baadhi ya wasanii kuhsu tuzo za EATV Awards kwenye mitandao ya kijamii.
Tags: