Nay wa Mitego.
Nay wa Mitego, aliyazungumza hayo Ijumaa kwenye kipindi cha Friday Night Live ya EATV na EA Radio baada ya kuulizwa kuhusiana na tetesi kwamba hapo awali alikuwa akitungiwa nyimba na rapa Kimbunga Mchawi kisha anapoziimba Kimbunga hurejea kutunga nyimbo kwa ajili ya kumjibu Nay wa Mitego.
Nay wa Mitego amesema kuwa kwa sasa yeye yupo juu kimuziki hivyo hawezi kujibishana kuhusiana na msanii Kimbunga Mchawi kwa kusema kuwa nikweli au si kweli kuhusu kumuandikiwa nyimbo hizo.