.jpg?itok=OmgQJlFE×tamp=1473705347)
Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa THTU Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Salifius G Mlingo amesema wamefurahishwa sana na hatua hiyo kwani tayari lugha ya Kiswahili inafundishwa katika nchi za Ghana, Libya, Zimbabwe, Namibia, Misri,Aljeria, Kenya na Uganda hivyo kuiweka lugha hiyo katika nafasi nzuri.
Nchi zingine kwa bara la Afrika amesema ni Burundi, Rwanda na Afrika Kusini huku akitaja nchi za nje ya bara la Afrika kuwa ni pamoja na China, Japan, Korea na India. Kwa bara Ulaya ni pamoja na Ujerumani, Italia, Uholanzi, Uingereza, Sweden, Ufaransa pamoja na Austria, na nchi zingine nyingi amesema Mlingo.
Mlingo amesema, licha ya jitijada hizo ni vyema serikali ikahakikisha kuwa tamko hilo linatekelezwa ipasavyo ambapo pia amependekeza kuwa n ivyema wachezaji wa mpira wa kitanzania, wasanii na wanamichezo mbalimbali wawapo nje ya nchi watumie Kiswahili kama lugha ya mawasiliano.