Alhamisi , 19th Mei , 2016

Wakala wa mabasi yaendayo kwa haraka nchini Tanzania -UDART imesema kuwa suala la watumishi wa umma wakiwemo walimu na polisi kupanda bure katika mabasi hayo bado halijafanyiwa utaratibu hivyo wataendelea kulipa kama watu wengine.

Meneja Uhusiano Mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) Bw. William Gatambi.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, jana Meneja Uhusiano wakala wa mabasi yaendayo haraka UDART, William Gatambi, amesema endapo watafanya hivyo italeta mchanganyiko kwa sababu mfumo uliopo hauruhusu mtu kupita bila kulipia.

Bw. Gatambi amesema kwa sasa wanatumia mfumo wa karatasi wakati wakiwa kwenye mchakato wa kuandaa mfumo wa tiketi za kieletroniki ambao wanaweza kufanya utaratibu ambao unaweza ukatoa nafasi kwa watumishi hao kupanda bure.

Aidha, Afisa Uhusiano huyo amesema katika kukabiliana na changamoto za foleni katika vituo hivyo wameamua kuzikata tikeki kabisa ili kusiwe na usumbufu kwa wasafiri wanaowahi kufika vituoni kwa sababu mara nyingine mtandao wa kutoa risiti unafanya taratibu katika utoaji risiti.

Aidha, amesema kuwa abairia hawana haja ya kukimbiala mabasi hayo hata kama limejaa kwa kuwa kupishana kwake yanachukua muda mfupi kituo kwa kituo hivyo ni vyema mtu kusubiri baada ya kuona gari limejaa.

Sauti ya Meneja Uhusiano Mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) Bw. William Gatambi,