Jumatatu , 25th Apr , 2016

Mwanadada anayetamba kwa ngoma yake ya NdiNdiNdi Lady JayDee amesema kwa kipindi chote ambacho anafanya muziki wa Bongo Flava hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii yeyote.

JayDee ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo wakati akizindua video ya NdiNdiNdi kwenye kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV.

Katika uzinduzi huo msanii huyo aliweka bayana kwamba ameandaa albam nzima ambapo ameanza kutoa single ya NdiNdiNdi na nyingine zitaendelea kutoka.

Aidha amewashukuru watu wote ambao wanaendelea kumuunga mkono katika kazi zake kwa muda mrefu sasa na kuahidi kwamba hatawaangusha.