Jumatatu , 7th Apr , 2014

Kundi la muziki la Mafikizolo ambalo usiku wa Jumamosi limefanya burudani ya aina yake Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mlimani City, wametoa ya moyoni kuwa, wamefurahishwa na kushangazwa na jinsi mashabiki wao hapa Tanzania wanavyowaelewa.

Mafikizolo jukwaani jijini Dar

Mafikizolo pia katika mahojiano maalum waliofanya na EATV, wameweka wazi mapenzi makubwa waliyonayo kwa Tanzania, na kufafanua zaidi juu ya mpango wao wa kufanya video moja nchini, ambapo wamesema wapo katika mipango ya awali na watatuma timu kwaajili ya kuangalia maeneo ambayo yatafaa kwaajili ya kupiga picha za video hii.

Wasanii hawa wamesema kuwa, video hii itakuwa ni ya nyimbo yao inayokwenda kwa jina Nakupenda, na vile vile wamesema kuwa hawakutarajia kuwa mashabiki wao hapa nchini wanaweza kuwa na ufahamu wa nyimbo zao zaidi ya Khona na Happyness.

Kwa kufahamu zaidi juu ya walichosema Mafikizolo, usikose kutazama shoo yako namba moja katika masuala ya fasheni na mitindo ya maisha, Nirvana inayokujia kila Jumanne saa moja kamili usiku.