Alhamisi , 15th Oct , 2015

Viva Concious, msanii anayefanya muziki chini ya Defatality Music, ameelezea namna anavyoweza kushika soko la muziki la hapa ndani na lile la kimataifa kwa wakati mmoja, moja ya mkakati ikiwa ni hatua yake ya kuachia rekodi mbili kwa pamoja.

Msanii wa muziki nchini Viva Concious kutoka lebo ya Defatality Music

Viva ambaye tayari amekwishaanza kueleweka sana nje ya mipaka ya nchi hususan nchini Sweden, akiwa sasa anatangaza kazi yake mpya ya Piga Chini, ameeleza pia kuwa licha ya ujumbe wa kazi hiyo kulenga vijana wa hapa, amewashirikisha wasanii wakali wanaotamba hapa, Stamina pamoja na Walter Chilambo.