Jumatatu , 21st Sep , 2015

Ikiwa ni sehemu ya mchango wa wasanii wa muziki hapa nchini siku ya leo wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Amani, wito umeendelea kutolewa kwa watanzania kuwa na amani hususan katika kuelekea kushiriki zoezi la uchaguzi mkuu tarehe 25 mwezi Oktoba.

Msanii nyota wa mashairi na pia msanii wa muziki nchini Mrisho Mpoto

Kwa niaba ya wasanii wengine, Nyota wa muziki Dayna, Nikki Wa Pili, Mrisho Mpoto kama pia moja ya jukumu lao kama kioo cha jamii wameeleza namna ambavyo katika nafasi zao wanakuwa mabalozi wa amani katika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.