Alhamisi , 27th Aug , 2015

Baada ya kufunguliwa kwa mashindano ya kumtafuta Miss Tanzania na Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA), Kamati ya Maandalizi ya Michuano hiyo imekuja na mikakati ya kurejesha mashindano hayo makubwa ya kusaka walimbwende nchini.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati Mpya itakayoratibu Mashindano ya Miss Tanzania katika mkutano na Waandishi wa Habari leo

Katika kuboresha mashindano ya Miss Tanzania, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga leo ametambulisha mbele ya waandishi wa habari kamati mpya yenye wajumbe 12, ambayo itakuwa inaratibu mashindayo hayo kwa sasa.

Wajumbe hao ni 1. Juma Pinto - Mwenyekiti
2. Lucas Rutta - makamu Mwenyekiti
3. Doris Mollel - Katibu Mkuu
4. Jokate Mwegelo - Msemaji wa Kamati
5. Hoyce Temu - Mjumbe
6. Mohamed Bawazir - Mjumbe
7. Gladys Shao - Mjumbe
8. Magdalena Munisi - Mjumbe
9. Shah Ramadhani - Mjumbe
10. Hamm Hashim - Mjumbe
11. Khalfan Saleh - Mjumbe
12. Ojambi Masaburi

Lundenga amesema kuwa kamati hiyo inayoanza kazi zake hii leo, itashughulikia mapungufu yote yaliyojitokeza na kurejesha imani ya wananchi kwa mashindano hayo ikishirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali pamoja na Basata.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jokate Mwegelo ametoa shukrani kwa niaba ya kamati yake kwa kuamininiwa kupewa jukumu hilo na kuahidi maboresho makubwa na mikakati endelevu ya kurejesha hadhi ya Miss Tanzania.