Jumapili , 23rd Aug , 2015

Msanii wa muziki Hisia ameanza maandalizi ya kufanya onesho lake kubwa la muziki alilolibatiza jina 'Muziki wa Hisia' litakalofanyika wiki ijayo mjini Arusha.

Msanii wa muziki wa miondoko ya Soul na RNB Hisia

Hisia ameongea na eNewz kuwa katika mfululizo wa maonesho yake hayo yanayotambulika kwa sehemu kubwa ndani na nje ya nchi, safari hii amewaunganisha baadhi ya wasanii wa muziki akiwemo mwanadada Maua Sama, Hemedi PHD na wengineo ambao watamsindikiza nyota huyo stejini siku hiyo.

Aidha naye Maua Sama amefurahia nafasi hiyo ya kutumbuiza na mkali huyo live na hii itakuwa ni mara yake ya kwanza kwa mwanadada huyo kutumbuiza naye katika onesho hilo kubwa Arusha.