Jumatano , 29th Jul , 2015

Usahili wa pili wa mashindano haya makubwa kabisaya Dance 100% 2015 utafanyika katika viwanja vya Don Bosco Upanga Jumamosi tarehe 01 Agosti mwaka huu, ambapo makundi mengine matano yatasakwa kuingia katika michuano hiyo kwa mwaka huu.

shindano kubwa la kucheza la Dance100%2015 jijini Dar es Salaam

Makundi hayo yataungana na yale yaliyokwishapatikana Temeke, Team ya Shamba, The WT Group, WD, The Best Boys Kaka Zao na Team Makorokocho, katika safari ya kuelekea usahili wa tatu na kisha robo fainali ya mashindano hayo makubwa ya kudansi nchini.

Kama amabavyo umekwishajionea mwanzo wa kishindo kabisa wa mashindano haya, Burudani na vipaji mwanzo mwisho, Jumamosi hii muelekeo utakua mmoja tu ni pale Don Bosco Upanga kuanzia saa nne asubuhi.

Pia usikose kutazama yote yaliyojiri katika usahili wa kwanza wa mashindano hayo kupitia shoo kali ya Dance100% 2015, siku ya jumamosi, kuanzia saa 12:30 jioni, hapa EATV pekee.