Mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Iringa Mjini Balozi Augustino Mahige.
Mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Iringa Mjini Balozi Augustino Mahige amesema wagombea wanaopata uongozi kwa kutumia rushwa wanashusha hadhi ya taifa.
Dkt. Mahige ameshauri kurekebisha sheria za rushwa kwani kwani suala hilo likiendelea linaweza kusababisha wawekezaji kuacha kuwekeza nchini na kuzorotesha maendeleo ya nchi.
Balozi Mahige amesema ikiwa atapata ridhaa ya kuongoza jimbo la Iringa Mjini ataboresha fursa za ajira kwa wananchi.
Amekishauri chama cha CCM kupunguza gharama za matumizi ya ziada ya mchakato wa kugombea nafasi hiyo kwani gharama zake ni kubwa zaidi ya ile ya kuchukua fomu
Jumla ya wagombea 13 wanashiriki katika kinyanganyiro hicho ambapo mchakato huo unashirikisha kata 18 katika manispaa ya Iringa.