Jumapili , 19th Jul , 2015

Mwadada anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki Tanzania akiwakilisha visiwa vya Zanzibar Baby J amesema baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu sasa mashabiki wake wakae tayari kwa ujio mpya.

Baby J akiwa katika pozi visiwani Zanzibar

Baby J ambaye muda mwingi yupo maskani yake Zanzibar amesema sababu ya kukaa zaidi ya mwaka bila kuachia ngoma mpaka watu wanadhani ameacha muziki ni matatizo binafsi ambayo yamekwishakaa sawa na sasa anarudi mzigoni.

Lakini Baby J hakutaka kuweka wazi jina la Project anayokuja nayo na kusema sasa yupo chini ya usimamizi ambao unamuongoza kwa hiyo soon mambo yatakua hadharani so funs wake wawe tayari kumpokea.