Jumatatu , 13th Jul , 2015

Msanii wa kike wa miondoko ya bongofleva ambaye anafanya vyema na video ya wimbo wake maarufu wa 'Nimempata' Pam Daffa atoa ya moyoni kuhusiana na uteuzi wa DK. John Pombe Magufuli.

Msanii wa kike wa miondoko ya bongofleva Pam Daffa

Pam D ameongea na eNewz akisema kuwa Magufuli amekuwa ni chaguo la wengi kutokana na uchapaji wake makini wa kazi na hii inamuweka katika njia safi ya kuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu mwaka huu.