Jumanne , 30th Jun , 2015

Mjumbe wa Mamlaka ya Taifa ya kupiga Vita Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya Kenya (Nacada) Charles Njagua maarufu kama Jaguar amedai kuwepo kwa uozo mkubwa wa rushwa katika mamlaka hiyo.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Jaguar

Jaguar ambaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Nacada karibu mwezi mmoja sasa, amesema amekuwa akikabiliwa na upinzani mkubwa kwa kuhoji upotevu na matumizi yasiyo sahihi ya fedha katika chombo hicho.

Akiongea katika mkutano kwenye ofisi Jaguar ambaye pia ni msanii wa muziki Kenya amedai kuwa wajumbe wa bodi ya Nacada na Kamati ya Fedha ni sehemu ya wahusika wa ubadhirifu wa fedha wa chombo hicho cha kupiga vita pombe na dawa za kulevya.

Jaguar amewatuhumu baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo kwa kuchota kiasi cha shilingi milioni 500 za Kenya bila ya kufanyiwa majadiliano na kuridhiwa na wajumbe wote wa bodi hiyo ya Nacada.