Jumatatu , 5th Feb , 2024

Nyota wa timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars", Simon Msuva ameripoti katika klabu yake mpya ya Al Najmah ya Saudi Arabia na kuanza mazoezi rasmi na kukutana na Viongozi wa timu hiyo.

Msuva alikuwepo katika kikosi cha Stars kilichoishia hatua ya makundi katika michuano ya AFCON 2023, nchini Ivory Coast.

Mshambuliaji huyo  wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva amejiunga na klabu ya Al-Najma yenye maskani Mji wa Unaizah inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia.

Msuva anajiunga na Al Najma kufuatia kuachana na JS Kabylie aliyojiunga nayo Agosti mwaka jana akitokea nyingine ya Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia, Al-Qadsiah aliyoichezea kuanzia mwaka 2022.