Jumanne , 7th Mar , 2023

Waziri wa Utamaduni, Sana na Michezo Mhe, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuendeleza mchezo wa Soka nchini itamlipa mshahara mwalimu wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),

kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Adel Amrouche

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa hafla ya  kumtambulisha Kocha huyo, Machi 07, 2023 Mtumba jijini Dodoma, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali inaamini Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limejiridhisha kuwa ni Kocha Bora atakayekuza soka la Tanzania.

" Ukitazama wasifu wa Kocha Adel utabaini uzoefu mkubwa alionao sio tuu katika kufundisha soka uwanjani, bali pia katika kuandaa Wataalamu wengine wa Soka, hivyo tumtumie vizuri ili asaidie timu yetu kufanya vizuri ndani na nje ya nchi"

Ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kuangalia uwezekano wa kupata wataalamu katika michezo mingine ambapo ameeleza kuwa Wizara inaendelea kuimarisha Wataalamu wa michezo kupitia Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichoko wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

Kwa upande wake Kocha Amrouche ameahidi kuwanoa  wachezaji vyema ili kuiweka juu zaidi  Tanzania katika ulimwengu wa Soka , huku akisisitiza ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali katika kufanikisha kazi