Alhamisi , 22nd Feb , 2024

Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF limeruhusu mashabiki kuingia bure kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki mashindano ya Olimpiki utaowakutanisha Timu ya Taifa ya wanawake “Twiga Stars”dhidi ya Afrika Kusini “Banyana Banyana”utaopigwa kesho ijumaa Februari 21, 2024 majira ya saa

Akitoa taarifa hiyo Afisa habari wa TFF Cliford Ndimbo amesema kuwa wale wote wenye nafasi ya kwenda uwanjani wajitokeze kutoa hamasa kwa timu ya taifa ya wanawake Tanzania, ‘’Twiga Stars’’ huku upande wao maandalizi yote yamekamilika ,

‘’Wanatamani kuona mashabiki wengine uwanjani ili kutoa hamasa kwa wachezaji nah ii inawasaidia katika kuongeza nguvu kwa wachezaji kuweza kupambana na hata kupata matokeo kwakuwa tupo nyumbani’’amesema Ndimbo .

Kwa upande wa makocha wa timu hizo za Taifa wamesema wamejiandaa vyema huku kila moja akitamba kupata matokeo nakujiweka katika nafasi nzuri ya kwenda kushiriki michuano hiyo ya Olimpiki inayotarajiwa kuanza mwaka huu nchini Ufaransa.