Taarifa hiyo imetolewa Jumatano ya Leo Oktoba 18, 2023 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro ambayo amepiga marufuku mashabiki kufanya vurugu wakati wa Kuingia Uwanjani ili kuhepuka usumbufu.
Kamanda Muliro ameendelea kwa kusema, Jeshi la Polisi halitovumilia tabia zozote zile zilizopigwa marufuku na FIFA, CAF na TFF ambazo zinaweza kupelekea Tanzania kukosa sifa ya kuandaa mashindano kama haya wakati mwingine kwani watakaokamatwa watachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa Upande Mwingine Kuelekea kwenye mchezo huo, Mashabiki wa Simba SC na Katibu wa matawi Simba SC Jijini Mwanza, wameelezea tambo zao za kupata ushindi dhidi ya Al Ahly utakaochezwa saa 12:00 Jioni Ijumaa Oktoba 20, 2023 kwenye dimba la Mkapa, Dar es salaam.