Alhamisi , 7th Nov , 2024

Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali yake ina mpango wa kujenga kiwanja cha mpira wa miguu cha kimataifa kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 zitakazofanyika nchi tatu za Afrika Mashariki.

Mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka wa 2027 yanatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa ushirikiano nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda ambazo ndizo zitakuwa  nchi wenyejiwa mashindano hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameendelea na ziara ya kikazi nchini China ambapo leo amekutana na kampuni mbalimbali zinazolenga kuwekeza Zanzibar. Katika mwendelezo wa ziara hiyo Rais Dk. Mwinyi pia, amekutana na uongozi wa kampuni maarufu na yenye uzoefu wa miaka mingi, China Railway Construction Engineering Group (CRJE), yenye makao makuu Beijing, China katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Westin, Shanghai, China.

Katika mkutano huo, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kujenga Mji wa Kiserikali ambapo Serikali na taasisi zake zitawekwa sehemu moja ili kuboresha ufanisi na utendaji serikalini pamoja na kurahisisha huduma kwa wananchi.

Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali yake ina mpango wa kujenga kiwanja cha mpira wa miguu cha kimataifa kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 zitakazofanyika nchi tatu za Afrika Mashariki.

Mkutano huo umekutanisha Benki na taasisi za fedha, wakiwemo wenyeji CRJE, China Dasheng Bank of Tanzania, Jiangsu Financial Leasing Co. Ltd, Huaxia Bank, Citic Bank, na Bank of Shanghai, ambao wamekuja kujadili fursa za uwekezaji na ushirikiano wa fedha katika miradi mbalimbali ya maendeleo Zanzibar.

Mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka wa 2027 yanatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa ushirikiano nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda ambazo ndizo zitakuwa  nchi wenyejiwa mashindano hayo.

Maandalizi yanaendelea kujiandaa na mashindano hayo ya mpira kwa mataifa ya Afrika ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, Hoteli pamoja na viwanja yanaendelea kwa kasi nchini Tanzania.Mpaka sasa Tanzinia kuna viwanja viwili vyenye hadhi ya kuchezwa kwa mashindano hayo Benjamini Mkapa Stadium na ule wa New Amaan Stadium ambao upo Zanzibar ( Tanzania visiwani).

Kiwamja kipya cha kisasa kinachojengwa Jijini Arusha ujenzi wake umefikia asilimia 6% na inakadiriwa utagharimu kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 200. Kiwanja hiko kikikamilika itafikisha idadi ya viwanja vitatu Tanzania vitakavyokuwa na hadhi ya kutumiwa kwenye michezo ya mashindano ya kimataifa kwa ngazi za klabu na nchi.

 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kujenga uwanja mpya wa kisasa kupitia Rais wa Zanzibar ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi uwanja huo utaongeza idadi ya viwanja vyenye hadhi ya kimataifa nchini na kuliweka taifa la Tanzania kwenye mazingira mazuri ya kupata uwenyeji wa mashindano mengine ya vilabu na mataifa yanayosimamiwa  na Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF.