Young killer
Young Killer amesema alikataa kufanya collabo na Young Tuso kwa sababu ailishafanya kolabo na mwisho wa siku hakuona wimbo huo ukitoka.
''Mimi sitaki ushabiki kwenye kazi ni lazima uwe na nidhamu kwenye kazi ili uweze kufanya vizuri. Anachofanya Young Tuso ni kutoheshimu muda wa mtu ila nilivyomkatalia kufanya collabo nyingine naamini akimuomba msanii mwingine atakuwa na heshima'', amesema Young Killer.
Lakini pia Young Killer ameiambia eNEWZ kwamba kitendo cha wimbo aliofanya na Young Tuso ambao mpaka leo haujatoka ndiyo kilichompelekea kukataa kufanya nae kazi nyingine.
Killer amemaliza kwa kuweka wazi kuwa alimshangaa sana alipoanza kusikia kuwa msanii huyo anajiita Mfalme wa Temeke bila kujali kuwa kuna akina Juma Nature na anaona kitendo hicho ni kuwavunjia heshima wakongwe hao.





