
Bao hilo la pekee limefungwa katika kipindi cha pili cha mchezo na mchezaji Hamis Tambwe dakika 83 kwa kupiga kichwa matata na kuifanya timu yake kuwa mbele kwa goli hilo mpaka kilipopulizwa kipenga cha mwisho cha muamuzi wa mchezo huo.
Kutokana na ushindi huo, timu ya Yanga imeweza kujiongezea pointi 3 na kufikia alama 68 na magoli 44 huku wapinzani wao wa jadi Simba SC wakishika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kwa pointi 65 na jumla ya magoli ya kufunga na kufungwa ikiwa ni 32 mpaka sasa.
Katika hatua nyingine, timu ya Simba itakuwa na kibarua kigumu endapo watahitaji kupata ubingwa katika msimu huu kwani watahitajika kushinda magoli zaidi ya 13 katika mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Mwadui FC.