Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa kukiripotiwa kuwa Yanga inakataa kusikiliza ofa za baadhi ya vilabu vikiwataka baadhi ya nyota wa timu hiyo wakihofia kudhoofika kwa kikosi cha wanajangwani hao ktu ambacho uongozi wa timu hiyo umekikanusha kwakua hakuna ombi wala ofa yeyote iliyowafikia kwa njia yoyote mpaka sasa.
Katibu mkuu wa timu hiyo Beno Njovu amesema kuwa mpira ni kazi ya mchezaji na kamwe hawatokua na pingamizi kama klabu inayomhitaji mchezaji yoyote wa klabu hiyo kwa kufuata taratibu.