Jumamosi , 13th Feb , 2016

Kikosi cha Yanga leo kinatarajia kushuka ugenini dimba la Geoge V nchini Mauritius kukipiga na Cercle de Joachim SC katika mchezo wa ligi ya klabu bingwa Afrika hatua ya awali.

Mabingwa hao watetezi wa kombe la ligi ya soka Tanzania bara wataoneshana kazi na wapinzani wao majira ya saa 16:30 kwa saa za Tanzania sawa na saa 15:30 kwa saa za Mauritius.

Yanga watacheza leo mchezo huo kisha kukwea pipa na kutimkia kisiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi ya kujifua kuwakabili watani zao wa jadi Simba SC katika mchezo wa marudiano wa ligi kuu utakaopigwa Februari 20 uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Jangwani kinachotarajiwa kuanza kwenye mchezo huo wa ugenini kinaongozwa na wachezaji wafuatao;

1. Ally Mustafa ‘Barthez’

2. Juma Abdul

3. Oscar Joshua

4. Kelvin Yondan

5. Vicent Bosou

6. Thaban Kamusoko

7. Saimon Msuva

8. Haruna Niyonzima

9. Donald Ngoma

10. Amis Tambwe

11. Deus Kaseke

Watakaoanzia benchi ni pamoja na;

Deogratius Munishi ‘Dida’

Pato Ngonyani

Haji Mwinyi

Juma Said Makapu

Paul Nonga

Issoufou Boubakar Garba

Matheo Anthony