Jumatatu , 17th Aug , 2015

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam ndani ya wiki hii kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya michuano ya ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC inayotarajiwa kupigwa Agosti 22 mwaka huu uwanja wa Taifa.

Vincent Bossou (kulia) akipambana na Didier Drogba wakati wa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN) mechi iliyokuwa kati ya Togo na Ivory Coast kwenye dimba la Royal Bofokeng Stadium Januari 22, 2013 Rustenburg, Afrika Kusini

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema, kikosi kitawasili huku wachezaji watatu Nahodha Nadir Canavaro, Ocsar Joshua na Amis Tambwe wakiwa katika mapumziko ya siku chache kutokana na kupatwa na maralia lakini watawasili kambini kuungana na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam FC.

Kwa upande mwingine Muro amesema, wameridhishwa na kiwango cha aliyekuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Togo Vincent Bossou na wamemsajili kwa mkataba wa miaka miwili.

Muro amesema, Bossou ataanza kuitumikia Yanga katika michuano ya ligi kuu na ya kimataifa, huku Yanga kwa upande wao wakiamini mchezaji huyo atapata muda ya kuzoeana na wenzie na ili kuijenga timu kuwa na mfumo wa pamoja ambao utatoa fursa kwa wachezaji wote kucheza kama kitimu.