Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Yanga SC Ally Kamwe ameweka wazi kuwa safari yao ya kwenda nchini Ethiopia inabebwa zaidi na malengo ya kuhakikisha wanakwenda kutafuta ushindi ili kufikia dhamira yao ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
''Malengo kwa sasa katika hatua hii kufika makundi imetuchukua miaka ishirini kufanya mambo mazuri kwenye timu yetu hivyo tunakwenda kushambulia na sikupaki basi''amesema Kamwe.
Kwa upande mwingine Kamwe ametolea ufafanuzi sababu za kwanini mchezaji wao mpya mshambuliaji Jean Baleke hatumiki kwenye michezo ya kimashindano.
Yanga ilifuzu raundi ya pili ya mtoano ya Ligi iya mabingwa afrika baada ya kufanikiwa kupita kwenye raundi ya awali ya mtoano kwa kuitoa timu ya Vital’O ya Burundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 10-0 kwenye mchezo wa mikondo miwili. Yanga ikifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla kwenye hatua hii itafuzu hatua ya makundi.