
Akizungumza na East Africa Radio, Meneja wa Timu ya Yanga, Hafidh Saleh amesema, wanatarajia kuondoka na kikosi cha wachezaji wote ikiwemo wale wageni ambapo kambi yao ya kwanza wataanzia Mbozi ambapo watacheza mechi ya kirafiki na Timu ya Kimondo inayoshiriki Ligi daraja la kwanza siku ya jumapili.
Hafidi amesema, baada ya kutoka Mbozi wataelekea Tukuyu kwa ajili ya kucheza mechi za timu mbili kutoka nje ya nchi ya kwanza ikiwa dhidi ya timu ya Zesco ya Nchini Zambia na Batter Bullets ya nchini Mlawi Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeyana baada ya hapo watarejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kujiandaa na mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Azam Fc.