
Kocha wa Stars Mkwasa akiwa na wachezaji wakiendelea na mazoezi Uwanja wa kituo cha michezo cha Edenvale.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hanspoppe amesema, wananchi wamekuwa na wepesi wa kusifia na kulaumu na lawama zao zinakuja kutokana na haraka ya kumpa kocha sifa kabla ya kujua timu ipo vipi.
Hanspoppe amesema, wananchi wasiangalie mechi moja au mbili za nyumbani pekee bali waangalie hata mechi za ugenini kwani ndiyo zinaonesha kiwango cha timu na sio kwa mechi moja pekee.
Hanspoppe amesema, kocha wa sasa ambaye ni mzawa Boniface Mkwasa anatakiwa kupewa nafasi kwani kuna kuteleza na kuna kurekebisha ili waweze kutoa maoni na mpaka zikifika mechi saba au nane kutakuwa na muelekeo.
Hanspoppe amesema, kwa sasa Stars inajiwinda dhidi ya timu ya taifa ya Algeria Novemba 14 mwkaa huu na hapo ndipo watanzania waangalie kiwango cha wachezaji wa Stars kwani Algeria ni timu ngumu na wataweza kuona muelekeo.