
Wanyama ameweka wazi hilo Jumamosi iliyopita kwenye kipindi cha Shabiki On Saturday cha East Africa Television alipokutana pamoja na mchezaji wa Tanzania anayechezea Diffa El Jadidi ya Morocco, Simon Msuva, ambaye alitaka kujua namna ya kufika alipofika Wanyama.
''Kikubwa ni kucheza kwa bidiii na kuwa na nidhamu ya hali ya juu huku ukiwa na njaa ya kufika juu zaidi huku ukisikiliza na kufuata vizuri maelekezo ya mwalimu, ila mimi huwa nikikutana na mawakala wakubwa huwa najaribu kuwaambia kuwa kuna mchezaji mzuri sehemu fulani jaribu kumfuatilia'', alisema.
Aidha Wanyama aliongeza kuwa yeye huwa anapenda kufuatilia zaidi wachezaji wa Afrika Mashariki wanaocheza nje na kufanya vizuri kwani anaamini nchi zote za ukanda huo ni wamoja na anatamani kuona siku moja nchi hizo zinacheza Kombe la Dunia.
Wanyama aliyewahi kucheza ligi kuu ya Ubeligji anakocheza Mbwana Samatta kabla ya kwenda Scotland na baadae England aliweka wazi kuwa ataendelea kuwa Tottenham na yupo kwenye mipango ya kocha Mauricio Pochettino.