
Timu ya wanawake ya kikapu ya Marekani
Wachezaji wao wawili wakongwe wa Marekani Sue Bird na Diana Taurasi wameingia katika orodha ya wachezaji wa kwanza kushinda medali tano za dhahabu katika mchezo wa mpira wa kikapu katika Olimpiki.
Kwa matokeo hayo ya Olimpiki Japan 2020, hii inamaanisha timu ya taifa ya Marekani haijashindwa kwenye michuano hiyo ya Olimpiki 55, ambapo mara ya mwisho kushindwa ilikuwa hatua ya nusu fainali mwaka 1992.