
Wakala wa wachezaji Jamal Kasongo amesema, wachezaji wanapofika mahala pa kujitambua kuwa wanataka kucheza soka nje umri wao unakuwa umeshapitiliza kwani umri unaotakiwa kwa mawakala wanaoshirikiana kutoka nchi za Ulaya ambao ni kuanzia miaka 17 mpaka 20 mpaka 21.
Kasongo amesema, nchi za Ulaya kwa mchezaji anayetokea nchi za Afrika wanatarajia akae miaka angalau miwili ili aweze kuendana na mazingira ya soka ya nchi husika au klabu husika ili kuhakikisha wanaweza pia kufanya biashara.
Kasongo amesema, mchezaji akishajua umri wake ni mkubwa anapunguza Umri lakini akishafika timu ya Taifa Umri unakuwa haupunguziki na wengine wanaaminika mara moja kutokana na kuwa na umbile dogo.
Kasongo amesema, sasa vilabu vinaanza kubadili suala la vijana kudanganya umri kwa kuwa na timu za vijana ambao wana uwezo mkubwa kisoka lakini vilabu vinatakiwa kuwafungulia milango vijana walionao.