Jumatatu , 20th Jun , 2016

Kama kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson kuna kitu atakuwa akijutia hajakiacha ndani ya klabu hiyo, ni Paul Pogba, aliyemuuza kwenda Juventus mwaka 2012, na sasa nyota huyo anatakiwa na miamba ya Ulaya Real Madrid kwa dau kubwa

Wakala wa Paul Pogba amebainisha kuwa ameanza mchakato wa mazungumzo na klabu ya Real Madrid kuhusu usajili utakaovunja rekodi ya dunia, kwenye kipindi cha kiangazi.

Nyota huyo wa Juventus yupo na kikosi cha Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2016, inayofanyika huko huko nchini mwao.

Wakala wa Mfaransa huyo, Mino Raiola amesema wapo kwenye mazungumzo ya awali na Real, na kama mambo yakienda sawa mchezaji huyo wa zamanai wa Manchester United atajiunga na miamba hiyo ya Hispania.

"Ndoto za Paul ni kushinda Ballon d'Or...na Real Madrid ni klabu nzuri kufanikisha hilo.