Jumatatu , 7th Mar , 2016

Chama cha kuogelea nchini TSA kumeahirisha zoezi la kuipitisha katiba yake siku ya Jumamosi baada ya kuchelewa kufikishwa katiba zotembili ya kiswahili na kiingereza zilizotakiwa kupitishwa.

Katibu Mkuu wa TSA Ramadhan Namkoveka amesema Jumamosi walikuwa na mkutano Mkuu kwa ajili ya kuzungumzia marekebisho ya katiba ya chama ambapo wajumbe wa mkutano Mkuu waliamua kuahirisha kupitishwa kwa katiba hiyo.

Namkoveka amesema, ndani ya wiki hii wanatarajia tena kukutana na kutoa maelezo ya jinsi ya kuipitisha katiba hiyo ikiwa ni pamoja na kuandaa katiba nyingine kwa luga ya kiswahili.