Jumanne , 31st Jan , 2017

Waamuzi wa Uganda wameteuliwa kusimamia mapambano ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika inayoanza Mwezi Februari mwaka huu.

Brian Miiro Nsubuga, aliyepangwa kuamua mechi ya Yanga

 

Kamati ya waamuzi ya CAF, imewateua, Mashood Ssali, Hussein Bugembe, Musa Balikoowa Ngobi na Ali Sabila Chelegat kwa ajili ya mchezo wa Zimamoto dhidi ya Ferroviara da Beira, ya Msumbiji, utakaopigwa Februari pili mwa huu, 2017.

Kwa upande wa Tanzania Bara, Alex Muhambi, Ronald Katenya, Okello Lee na Brian Miiro Nsubuga wameteuliwa kusimamia mchezo wa Yanga dhidi ya Ngaya Club De Mde, ya Comoro, wikiend ya Februari 17 -19, 2017.