Jumatano , 26th Aug , 2015

Mabingwa wa Kombe la Kagame Timu ya Azam FC imesema wanaendelea na mazoezi huku ikiwa na wachezaji pungufu kutokana na baadhi ya wachezaji wa kimataifa na wa ndani kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa.

Akizungumza na East Africa Radio Afisa Habari wa Azam FC Jaffar Idd Maganga amesema, wachezaji walioitwa na timu zao za Taifa ni Jean-Baptiste Mugiraneza ameitwa na timu yake ya Taifa ya Rwanda, Didier Kavumbagu akiwa na timu yake ya Taifa ya Burundi na Allan Wanga akiwa kaitwa na timu yake ya Taifa ya Kenya.

Maganga amesema, baadhi ya wachezaji wametolewa kwa mkopo kutokana kukosa nafasi hivyo wameenda kukuza vipaji vyao katika timu hizo.

Maganga amesema, licha ya wachezaji hao kuchukuliwa kwa mkopo na timu hizo lakini hawataweza kucheza mechi baina na Azam FC lakini Klabu hizo zimetakiwa kuwakatia wachezaji hao bima ya matibabu ambapo watatakiwa kutibiwa kama wachezaji wa Klabu kubwa.