Ijumaa , 7th Mar , 2014

Vyama vya michezo ambayo itashiriki michuano ya madola vimekumbushwa kufanya kazi kwa umakini katika kuelekea michuano ya jumuiya ya madola ambapo

Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC imesema kuwa maandalizi ya michezo ya jumuiya ya madola kwa vyama vya michezo nchini yamekua ya kusuasua pamoja na TOC kuwakumbusha mara kwa mara kwa njia mbalimbali

Katibu mkuu wa TOC Filbert Bayi amesema kuwa awali walishaviandikia barua vyama vyote 8 kuomba taarifa za wachezaji wao wanaojiandaa kwa michezo ya jumuiya ya madola Glascow 2014 kuleta taaarifa hizo lakini hakuna chama kilichofanya hivyo

Wakati huo huo Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC imepongeza hatua ya serikali kupitia kwa wizara ya mambo ya nje kwa kutoa fulsa kwa wanamichezo mbalimbali watakaoshiriki michuano ya jumuiya ya madola kwenda kujiandaa nje ya nchi

Katibu mkuu wa TOC Filbert Bayi amevitakaka vyama hivyo vya michezo ya riadha, ngumi, judo na mpira wa meza kutumia fulsa hiyo ya waziri Membe kupeleka wachezaji vijana kwa faida ya baadae.